IQNA

Walowezi wa Kiyahudi wavamia msikiti wa al Aqsa

12:05 - April 15, 2009
Habari ID: 1765259
Walowezi 130 wa Kizayuni wameingia katika uwanja wa msikiti mtukufu wa al Aqsa wakiandamana na askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Duru za Palestina zimeripoti kuwa wakati wa kuingia katika uwanja wa msikiti huo, askari wa Kizayuni wa Israel walimtia nguvuni Muislamu mmoja aliyekuwa akitekeleza ibada ya swala msikitini hapo na kumpeleka kusikojulikana.
Siku chache zilizopita Mshauri wa Waziri Mkuu wa Palestina katika Masuala ya Quds Tukufu Bi Abdulqadir alizungumzia uwezekano wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia msikiti wa al Aqsa na akatangaza kuwa hatua hiyo inachukuliwa kwa kisingizio cha sherehe za Kiyahudi za siku eti ya kuzaliwa taifa la Mayahudi.
Bi Abdulqadir ametahadharisha kuhusu natija na athari mbaya za harakati hizo za Wazayuni. Mshauri wa Waziri Mkuu wa Palestina amewataka wakazi wa Baitul Muqaddas na Waarabu wa Israel kuzuia mashambulizi ya aina yoyote ya jeshi la utawala haramu na Mayahudi wenye misimamo mikali dhidi ya msikiti wa al Aqsa. 388106

captcha