IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani nchini Kuwait

12:25 - April 16, 2009
Habari ID: 1765620
Muhammad Abdul Ghaffar as-Sharif, Katibu Mkuu katika Wizara ya Wakfu ya Kuwait amesema kuwa sekreterieti ya wizara hiyo iko tayari kuandaa duru ya 13 ya mashindano ya taifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya tajweed. Mashindano hayo yatasimamiwa na Mfalme Ahmad as-Swabah wa nchi hiyo.
As-Sharif amesema kuwa huo ndio mpango mkubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na wizara hiyo ya Wakfu. Amesema lengo la mashindano hayo ambayo yatawashirikisha watu wa umri tofauti ni kuwahamasisha Wakuwait washiriki katika mashindano ya kuhifadhi kusoma na kutadabari katika maana ya Qur'ani Tukufu na pia kuwasilishwa mafundisho ya kitabu hiki kitakatifu kama njia bora zaidi ya maisha.
Vilevile amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuimarisha thamani za Kiislamu katika jamii na kuyasaidia makundi yanayojishughulisha na masuala ya mafunzo ya Qur'ani yaweze kufikia malengo yao.
Amesema idadi ya watu wanaoshiriki katika mashindano hayo yanayoungwa mkono na viongozi wa ngazi za juu zaidi wa serikali inaongezeka kila mwaka. 388808
captcha