IQNA

Majaji wa mashindano ya Qur'ani kuwa na kipimo kimoja

12:28 - April 16, 2009
Habari ID: 1765629
Jumuiya ya Darul Qur'ani ya Iran imeanzisha mafunzo ya muda ya majaji wa mashindnao ya Qur'ani ili majaji wote watumie mbinu moja kutathmini usomaji wa washindani na kuzuia utumiaji wa maamuzi ya mtu binafsi katika kutoa hukumu za mashindano hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Darur Qur'ani Hussein Behbudi amesema kuwa kutumiwa kwa timu moja ya majaji katika mashindano ya Qur'ani ya mwaka jana kulipelekea kupuuzwa matumizi ya mbinu za aina moja katika kutathmini na kutoa hukumu kwenye mashindano hayo. Hussein Behbudi amesema kwamba kuna upungufu wa majaji wenye uzoefu wa mashindano ya Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa miongoni mwa malengo ya mafunzo ya muda ya majaji wa Qur'ani ni kutayarisha majaji wenye uzoefu wa kutosha, kujitosheleza katika uwanja huo katika ngazi za mikoa, kuweka vigezo sawa vya mbinu za kutoa hukumu na kutathmini mashindano mbalimbali ya Qur'ani na kadhalika.
Amesisitiza kuwa wahitimu wa masomo hayo watapewa shahada za kuhitimu mafundisho ya ujaji wa mashindano ya Qur'ani. 389103
captcha