Oustaz Cheikh Seck, Imam wa Swala ya Ijumaa ya mji huo na ambaye pia ni miongoni mwa watayarishaji wa maonyesho hayo ameashiria umuhimu wa maonyesho hayo na kusisitiza kwamba yametayarishwa ili kuarifisha masuala ya kielimu na kidini ya waandishi wa Kiarabu na Kiislamu na hasa wa Senegal kwa wanafunzi na watafiti wa masuala ya kielimu ili waweze kufikia kirahisi marejeo ya kuwawezesha kunyanyau viwango vyao vya maarifa na elimu. Amesema pia vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kisenegali na ambavyo vimetarjumiwa kwa lugha za Kiarabu na Kifaransa pia vitaonyeshwa katika maonyesho hayo. 389538