Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria Sana, kamati hiyo imetoa taarifa ikisema kuwa kikao hicho kimefanyika kwa madhumuni ya kuunga mkono mapambano ya kishujaa ya watu wa Palestina katika kukabiliana na maghasibu wa utawala haramu wa Israel ulioazimia kufuta na kuharibu kabisa utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa mji wa Baitul Muqaddas kwa maslahi na manufaa ya Mayahudi na Wazayuni walioghusubu mji huo.
Taarifa hiyo imelaani kwa maneno makali hatua hizo za uharibifu za utawala wa Kizayuni na kusema kuwa Kamati ya Wananchi ya Kuadhimisha Quds Tukufu, Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Kiarabu katika mwaka 2009 imechukua hatua ya kuandaa siku ya kufungamana na taifa la Palestina ili kukabiliana na marufuku iliyowekwa na utawala huo haramu dhidi ya kufanyika sherehe za aina yoyote ile za kuadhimisha mji mtukufu wa Quds kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa nchi za Kiislamu. Kamati hiyo imesema, siku hii ilipaswa kuadhimishwa katika miji mikuu yote ya nchi za Kiarabu na Kiislamu ili kuonyesha mfungamano wao na taifa la Palestina.
Kwa msingi huo, Maputo au mabaluni yaliyokuwa yamechorwa na kupakwa rangi ya bendera ya Palestina yalipeperushwa katika anga ya miji kadhaa mikuu ya nchi za Kiislamu na Kiarabu zikiwemo za Algeria, Syria, Lebanon, Misri na Afrika Kusini. Vilevile vikao vingine vinavyohusiana na historia ya Quds Tukufu na mustakbali wa mji huo ni miongoni mwa ratiba nyingine zilizoandaliwa na kutekelezwa kwa mnasaba wa siku hiyo. 389617