IQNA

Mkutano wa vyuo vikuu duniani kufanyika mwishoni mwa mwezi huu

12:10 - April 18, 2009
Habari ID: 1766252
Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu (FUMI) inatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu AIU unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 hadi 22 katika mji wa Gadalajara nchini Mexico.
Mkutano huo ambao utahudhuriwa na jumuiya na taasisi 60 za vyuo vikuu duniani, utajadili masuala mbalimbali kuhusu mustakbali wa vyuo vikuu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu Mustafa Ahmad Ali pia atahudhuria mkutano huo wa tatu wa taasisi hiyo. 389933
captcha