IQNA

Kikao cha pili cha Ubunifu wa Fikra ya Kidini kufanyika

9:04 - April 19, 2009
Habari ID: 1766600
Kikao cha pili cha Ubinifu wa Fikra ya Kidini kitafanyika mwezi Novemba kwa uandalizi wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika Vyuo Vikuu. Lengo la kikao hicho ambacho kitafanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti hapa mjini Tehran ni kueneza misingi ya fikra za Kiislamu, jukumu ambalo watalitekeleza wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka katika vyuo vikuu vya masomo ya kawaida na vya masomo ya kidini.
Abu Talibi mmoja wa wakuu wanaoandaa kikao hicho amesema kuwa moja ya malengo ya kufanyika kikao hicho ni kutekeleza sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na umuhimu wa kuwasilishwa fikra mpya za Kiislamu katika masuala ya utafiti na sayansi katika vyuo vikuu. Amesema watu walio na hamu ya kuwasilisha makala katika kikao hicho wanaweza kutumia anwani ifuatayo: Hamayesh@sbu.ac.ir.
Mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na utambulisho, mipaka, fikra mpya za kidini katika zama mbalimbali na utekelezwa wa sheria za kidini katika zama hizo, fikra mpya za kidini katika vyuo vikuu vya kidini na visivyo vya kidini, athari za fikra mpya za kidini, udharura wa fikra mpya za kidini na fikra mpya za kidini na fikra za Magharibi.
Watu walio na hamu ya kushiriki kupitia makala wanaweza kuwasilisha makala zao hadi kufikia tarehe 21 Agosti.
Kikao cha kwanza kama hicho kilifanyika tarehe 15 Disemba mwaka uliopita katika ukumbi wa chuo hichohicho cha Beheshti. 390151
captcha