IQNA

Kutangazwa siku ya kufungamana na Quds nchini Lebanon

9:09 - April 19, 2009
Habari ID: 1766601
Sherehe maalumu za Siku ya Kufungamana na Quds Tukufu zilizoandaliwa na Harakati ya Wananchi ya Kuadhimisha Quds; Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiarabu zimefanyika katika makao makuu ya Shirika la Masuala ya Kijamii na Kiuchumi la Nchi za Magharibi mwa Asia ambalo linafungamana na Umoja wa Mataifa, mjini Beirut Lebanon.
Kwa mujibu wa IQNA kutoka Beirut, sherehe hizo zilihudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi na wanafikra wa Lebanon, Syria na Palestina.
Huku wakipeperusha bendera za Palestina, washiriki katika sherehe hizo walitangaza kwa sauti moja uungaji mkono wao kwa taifa madhlumu la Palestina. Akizungumza katika sherehe hizo, Hisham Ya'quub Mkuu wa Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Shirika la Quds aliwataka washiriki kuwaunga mkono kwa dhati wananchi wa Palestina wanaodhulumiwa kila uchao na utawala haramu wa Israel na pia kufanya juhudi za kuvunja mipango na njama za utawala haramu wa Israel za kufuta utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa Quds Tukufu.
Kwa upande wake, Asad Dayab, Mkuu wa Shirika la Kiutamaduni la Kiarabu la Lebanon amesema kuwa njia pekee ya kuikomboa Quds ni kupitia mapambano na umoja wa Waislamu na kuongeza kwamba, Quds kamwe haiwezi kukombolewa kupitia hitilafu zinazochochewa na Wazayuni miongoni mwa Waislamu. Amesema kuwa ushirikiano wa Waislamu na Wakristo katika kukomboa eneo hilo takatifu ni miongoni mwa juhudi kubwa zinazopaswa kutekelezwa na watu wote wanaopigania haki za Wapalestina na utukufu wa eneo hilo. 390128
captcha