Katika kitabu hicho mwandishi huyo mashuhuri wa Bulgaria amesisitiza kwamba zaidi ya raia milioni moja wa Bulgaria ni Waislamu na kwamba wafuasi wa dini nyingine hawajui vizuri mafundisho ya dini ya Kiislamu na ufahamu wao kuhusu dini hiyo unaishia katika masuala ya kijuujuu na yasiyokuwa ya kweli.
Radko Bobov Amesema kuwa Qur'ani tukufu imemtaja Bi Maryam mara 34 na kwamba hadithi nyingi za Mtume Muhammad (saw) na vitabu vya Kiisalmu vimemtaja kwa wingi mtukufu huyo.
Bobov amesema kuwa anatarajia kwamba kitabu cha Masih katika Qur'ani kitasaidia kuondoa taswira isiyokuwa sahihi kuhusu dini tukufu ya Kiislamu na kuwa mwanzo mzuri wa maelewano kati ya wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo.
390069