IQNA

Isesco kuandaa kikao cha malezi ya Kiislamu nchini Uswisi

16:26 - April 19, 2009
Habari ID: 1766960
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limepanga kuandaa kikao cha malezi ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu tarehe 23 hadi 26 mwezi huu wa Aprili nchini Uswisi.
Kwa mujibu wa gazeti la Tishrin la Syria, walimu na wataalamu wa masuala ya malezi 38 kutoka nchi za Italia, Ujerumani, Norway, Ufaransa na maeneo mbalimbali ya Uswisi wamealikwa kushiriki katika kikao hicho ambacho kimepangwa kufanyika katika mji wa Neuchatel.
Lengo la kikao hicho ni kujadili njia za kufunza malezi ya Kiislamu, kuwaelimisha walimu kuhusiana na malezi ya Kiislamu, kuwapa mafunzo na maelezo zaidi kuhusiana na masuala ya kielimu na kuwafahamisha washiriki kuhusiana na athari za utamaduni wa Kiislamu katika malezi ya watoto wa Kiislamu.
Mbinu mpya katika malezi ya Kiislamu, vikwazo vya malezi ya Kiislamu kwa msingi wa masuala yanayojitokeza katika zama hizi na sifa za utamaduni wa Kiislamu ni malengo mengine ya kuandaliwa kikao hicho. 390367
captcha