Muhammad Fenish amesema kuwa iwapo kulisaidia taifa la Palestina na juhudi za kurejesha amani nchini humo ni kosa la jinai basi Hizbullah inakiri kufanya kosa hilo kwa sababu inaamini kwamba amani na utulivu wa Palestina una mfungamano na usalama wa nchi za Kiarabu.
Waziri wa Kazi wa Lebanon amesema kuwa wale wanaodhani kwamba usalama wao unahatarishwa na jihadi na mapambano ya vijana wa Lebanon ya kuwatetea Wapalestina wanaokandamizwa, wanapaswa kuelewa kwamba Israel inafanya kila iwezalo kuvuruga amani na usalama huo.
Amesema kuwa vijana wa Kiislamu wanauawa shahidi kwa kosa la kuwatetea na kuwapelekea misaada wananchi wa Ukanda wa Gaza.
Amesema kuwa mahasimu wanaojiuza kwa vijidola kadhaa au kwa ajili ya kupata radhi za mabwana zao wa Magharibi wanataka kuyadhihirisha mapambano ya kupigania haki na viongozi wake kuwa hawana maana na thamani yoyote.
Muhammad Fenish amesema kuwa wanamapambano wa Hizbullah wamefanikiwa kukomboa ardhi za Palestina kutoka kwa maghasibu wa Kizayuni na Hizbullah inakutambua kuwasaidia wananchi wa Palestina kuwa ni wajibu wake wa kibinadamu. 390762