IQNA

Kituo kipya cha Qur'ani chafunguliwa katika mkoa wa Aqaba

15:00 - April 21, 2009
Habari ID: 1768034
Kituo kipya cha Qur'ani Tukufu kimefunguliwa katika mkoa wa Aqaba nchini Jordan ikiwa ni katika jitihada za kueneza zaidi utamaduni wa Qur'ani.
Mwandishi wa IQNA nchini Jordan amemnukuu Mkurugenzi wa Idara ya Waqfu ya eneo la Aqaba akisema kuwa kituo hicho cha Qur'ani kitaanza kazi katika siku chache zijazo na kutoa mafunzo ya Qur'ani katika nyanja mbalimbali.
Sulaiman Bulbul amesema, kwa sasa mkoa huo wa Aqaba una vituo sita vya Qur'ani kwa ajili ya wanaume na saba makhsusi kwa ajili ya wanawake. Amesema kuwa vituo hivyo vinatoa masomo ya sheria za tajwidi, elimu ya hadithi, fiqhi na sira ya Mtume Muhammad (saw).
Mkurugeni wa Idara ya Waqfu ya Aqaba amesema kuwa inatazamiwa kuwa katika msimu wa joto wa mwaka huu kutafunguliwa vituo 150 vya kusoma na kuhifadhi Qur'ani katika mkoa huo. 391474


captcha