IQNA

Msomaji elektroniki, mbinu mpya ya kufunza Qur'ani

11:21 - April 22, 2009
Habari ID: 1768397
Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhisha Qur'ani nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza imebuni mbinu mpya ya kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu iliyopewa jina la Msomaji Elektroniki.
Kituo cha habari cha al Masriyyun kimeripoti kuwa mbinu hiyo imebuniwa kwa shabaha ya kupanua zaidi shughuli za Qur'ani Tukufu katika upeo wa kimataifa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri na Kuhifadhisha Qur'ani nchini Saudia Aidha al Ufi amesema kuwa hii leo mtandao wa intaneti umekuwa wenzo unaoweza kutumiwa kwa wepesi na uwanja nzuri wa kueneza mafundisho ya Qur'ani. Amesisitiza kuwa jumuiya hiyo ina walimu 2900 wa Qur'ani wa kiume na 2800 wa kike wanaotoa mafunzo ya kitabu hicho kitukufu kwa njia ya intaneti.
Aidha al Ufi amesema kuwa vituo vya mafunzo ya Qur'ani katika mtandao wa intaneti ni moja ya njia za kuwaamsha vijana wa Kiislamu na amesisitiza juu ya kutumiwa teknolojia ya kisasa na walimu wenye uzoefu katika kuimarisha uhusiano wa vijana na kitabu cha Qur'ani. 392175

captcha