Kwa mujibu wa gazeti la al-Madina linalochapishwa nchini Saudi Arabia, sherehe hizo zimeandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Saudi Arabia kwa lengo la kuwashajiisha wasichana wajishughulishe na masuala ya Qur'ani. As-Sheikh Hamud bin Atiq al-Maabadi, mmoja wa wakuu walioandaa sherehe hizo amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, sherehe hizo zitajumuisha visomo vya watu waliohifadhi Qur'ani, hotuba za watu waliohitimu masomo yao katika jumuiya hiyo, kuwasilishwa rekodi ya shughuli zilizotekelezwa na jumuiya hiyo pamoja na kutolewa zawadi kwa watu waliofanya vyema katika uhifadhi wa Qur'ani Tukufu. 392883