Shirika la habari la Tunisia (TAP) limeripoti kuwa mkutano huo wa siku nne unasimamiwa na Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia ya Tunisia kwa lengo la kustawisha mazungumzo kati ya tamaduni na dini mbalimbali.
Malengo mengine ya mkutano huo yametajwa kuwa ni pamoja na kutetea amani na uadilifu na kutumia thamani za kimataifa kwa ajili ya kuimarisha maelewano kati ya watu na nchi mbalimbali.
Watafiti, maulamaa wa kidini, wataalamu wa masuala ya binadamu na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi 48 za Kiislamu, Afrika na America wanajadili na kubadilishana mawazo kuhusu maudhui za amani na uadilifu katika Qur'ani Tukufu, suna za Mtume Muhammad (saw) na haki za binadamu na historia ya amani na uadilifu katika fikra za kifalsafa. 392136