Kwa mujibu wa gazeti la al-Jazeera linalochapishwa mjini Riyadh, mashindano hayo yataendelea kwa muda wa siku kumi katika hoteli ya al-Izdihar Huleidi katika mji huo.
Abdul Aziz bin Adbul Rahman, Katibu wa Mashindano ya Qur'ani katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, baada ya kupita miaka 11 tokea kufanyike duru ya kwanza ya mashindano hayo, mashindano ya hivi sasa yameshuhudia mapokezi makubwa zaidi ya washiriki. Amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika hatua tatu tofauti za kieneo, kimkoa na kitaifa.393668