IQNA

Kikao cha kimataifa cha Mbinu za Tafsiri ya Qur'ani chamalizika Algeria

15:38 - April 25, 2009
Habari ID: 1769264
Kikao cha kimataifa cha Mbinu za Tafsiri ya Qur'ani kilichohudhuriwa na wasomi na wataalamu kutoka nchi Misri, Syria na Algeria kimemaliza kazi zake katika mkoa wa Um al Bawaqi huko Algeria.
Mkutano huo ambao ulisimamiwa na Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya al Furqan, ulichunguza mbinu mbalimbali za kufasiri Qur'ani na jinsi ya kuondoa makosa ya baadhi ya mbinu hizo.
Msomi Muhammad Hassan kutoka Misri ambaye amezungumzia mada ya "Mbinu ya tafsiri ya maswahaba wa Mtume (saw)" katika mkutano huo amesisitiza juu ya udharura wa kufanywa mlinganisho kati ya tarjumi za sasa za Qur'ani na zile za zama za awali za Uisalmu.
Sheikh Muhammad Hassan ameashiria kuwa kufasiri Qur'ani Tukufu kunahitaji nyenzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukifahamu vyema kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na hadithi za Mtume Muhammad (saw), na akasema kuwa ujumbe wa Qur'ani ni kwa ajili ya wanadamu wote na kwamba wanapaswa kutaamali ndani ya kitabu hicho.
Baadhi ya maudhui zilizojadiliwa katika mkutano huo wa kimataifa ni pamoja na "mbinu mpya za tafsiri", "tafsiri ya maudhui makhsusi" na uchambuzi wa muundo wa Qur'ani Tukufu". 393459

captcha