IQNA

Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Senegal

10:38 - April 25, 2009
Habari ID: 1769267
Serikali ya Senegal imeazimia kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu kitakachofadhiliwa na Saudi Arabia. Chuo hicho kitajengwa katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Dakar.
Waziri wa Elimu ya Juu ya Senegal Moustapha Sourang amesema kuwa chuo hicho cha Kiislamu kitajengwa katika eneo la Diamniadio pamoja na serkondari ambayo itajengwa katika eneo la Keur Massar.
Waziri Sourang amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo utagharamiwa na Wizara ya Masuala ya Kidini ya Saudia.
Amesisitiza kwamba Senegal pia inajenga Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kiislamu. 393551


captcha