Kwa mujibu wa Ofisi ya Uhusiano wa Umma katika Haram hiyo, CD za maqari mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu umekusanya visomo sita vya Ustadh Ahmad Amar, visomo vitano vya Ustadh Rafa'at na visomo 52 vya Ustadh Manshawi pamoja na makumi ya visomo vya maustadhi wengine wakubwa wa Quran kutoka kote duniani.
Katika benki ya kanda ya Haram Takatifu la Abdul Adhim al Hassani (AS) mjini Tehran, kuna mamia kwa mamia ya kanda na CD za sauti na taswira.
CD hizo zinajumuisha pia Tartili mbalimbali za Quran Tukufu, aina za Qasida na adhana za waadhini kutoka kona zote za dunia na pia kuna CD za hafla za kidini zilizofanyaika katika haram hiyo tukufu. Aidha benki hiyo ya sauti na taswira inazo CD za tilawa za maustadhi mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu kama vile Moustafa Ismail, Mohammad Siddiq Manshawi, Abdulbasit Muhammad Abdulswamad, Muhammad Ali Al Banna, Shahat Mohammad Anwar, Raghib Mustafa Ghalwash, Ahmad Naina'a, Abdulaziz Hisan, Abulaenein Shaishai, Abdulqadir Sahishai pamoja na maqari bingwa Wairani.
Benki hiyo ya CD iko wazi kwa watu wote wanaozuru Haram Takatifu la Abdul Adhim al Hassani (as) mjini Tehran.
393984