IQNA

Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran:

Wamagharibi ni warongo katika madai ya kutetea uhuru wa kusema

9:27 - April 26, 2009
Habari ID: 1769730
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran amesema kuwa Wamagharibi hawako tayari kusikia maneno ya haki kutoka kwa mtu yeyote na utendaji na mweneno wao unaonyesha kwamba ni warongo katika madai yao eti ya kutetea uhuru wa kusema.
Muhammad Mahdi Zahidi, Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran ameashiria hatua ya baadhi ya wanadiplomasia wa Magharibi ya kuondoka katika mkutano wa kupiga vita ubaguzi mjini Geneva wakati Rais Ahmadinejad alipokuwa akihutumia mkutano huo na akasema, Wamagharibi wameonyesha kuwa licha ya kutoa kaulimbiu za uhuru wa kusema lakini wao wenyewe ndio wapinzani wakubwa wa uhuru huo.
Amesema kuwa Wamagharibi walipaswa kusikiliza maneno ya Rais Ahmadinejad na kisha kuyakosoa kama walikuwa na neno la kusema.
Waziri wa Sayansi wa Iran amesema Wamagharibi hawakuwa tayari hata kusikiliza maneno na mtu mwingine jambo linaloonyesha kwamba ni warongo katika madai yao ya kutetea uhuru wa kusema. Muhammad Mahdi Zahidi ameongeza kuwa katika mkutano wa Geneva Rais wa Iran aliwalingania walimwengu kupigania uadilifu, kujali na kuthamini masuala ya kiroho na thamani za kibinadamu na kupambana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema aliwataka walimwengu kujenga dunia mpya isiyokuwa na ubaguzi ambamo uadilifu utakuwa na nafasi kubwa zaidi ndani yake. 394050

captcha