Hayo yamesemwa na Imam wa Swala ya Ijumaa ya Mash'had kaskazini mwa Iran Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Baqir Farzaneh. Ameongeza kuwa zilzala ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ilitetemesha tawala za kidhalimu duniani na kuwatia wahaka viongozi wa tawala hizo. Sheikh Baqir Farzaneh amesema kuwa nchi za Magharibi zilifanya na zinafanya jitihada na njama kubwa za kukwamisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran zikiwemo za kutumia nguvu za kijeshi na kwamba moja ya mifano ya njama hizo ni vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran.
Hujjatul Islam Farzaneh amesema kuwa chaguo la kutumia nguvu za kijeshi limeshindwa mbele ya Iran, Lebanon, Palestina, Iraq na Afghanistan.
Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa ya Mash'had amesema kuwa maendeleo makubwa ya Iran katika medani ya teknolojia yameharibu ndoto ya kuhodhi sayansi na elimu ya nchi za Magharibi. 393907