IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Wales

10:34 - April 27, 2009
Habari ID: 1770123
Jumuiya ya Kiislamu ya Wales nchini Uingereza imepanga kuandaa mashindano ya Qur'ani Tukufu tarehe 6 na 7 za mwezi wa Juni.
Kwa mujibu wa tovuti ya NWIS katika mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika katika msikiti wa mji wa Bangor huko Wales, washindani watashindana katika sehemu mbili za kuhifadhi sura za Baqarah na Aal Imran. Kila sehemu itakuwa na washindi watano ambao watachaguliwa kutokana na kasi yao ya kusoma sehemu watakayoainishiwa na ufahamu wao wa maana ya aya zinazosomwa na pia usomaji sahihi wa tajweedi.
Kila mshindi wa suratul Baqara atapewa zawadi ya laptop na kila mshindi wa suratu Aal Imran atazawadiwa iPod ambayo itakuwa na hifadhi ya Qur'ani Tukufu ya visimo vya wasomaji watano bora wa ulimwengu wa Kiislamu, wakiwemo Abdul Basit, al-Huswari na Manshawi. 394583
captcha