IQNA

Kikao cha kuipa miji utambulisho wa Kiislamu chafanyika Tehran

10:37 - April 27, 2009
Habari ID: 1770297
Kikao cha ‘Kuipa Miji Utambulisho wa Kiislamu’ kimefanyika katika Kituo cha Masomo ya Ukurugenzi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Tehran.
Kongamano hilo lilofanyika 26 Aprili lilitayarishwa na wanachama wa Jumuiya ya Wataalamu wa Quran Tukufu katika Taasisi ya Harakati za Quran ya Wanachuo nchini Iran.
Katika kongamano hilo, Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyed Samamudin Qavami mtaalamu mwandamizi wa masuala ya kidini alitathmini namna ya kuipa miji utambulisho wa Kiislamu. Kikao hicho ni cha nne katika silisili ya vikao vitakavyofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao. 394292
captcha