Ayatullah Muhsin Mujtahed Shabestari ameashiria nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu harakati za kuelekea katika marekebisho ya kigezo cha matumizi na kusema, 'waliokusudiwa mwanzo katika suala la kurekebisha kigezo cha matumizi ni wakurugenzi na maafisa wa serikali kisha wananchi'.
Ayatollah Shabestar amesema: 'Matumizi yanapaswa kuenda sambamba na hadhi ya jamii ya Kiislamu na jamii haipaswi kujitumbukiza katika israfu'.
Imamu wa Ijumaa mjini Tabriz amesema idhini ya kuingiza baadhi ya bidhaa kutoka nchi za kigeni imetoa pigo kwa viwanda vya ndani ya nchi na kusema suala hili linahusiana moja kwa moja na marekebisho ya kigezo cha matumizi.
Ayatollah Shabestari amesema, kuna haja ya kubuniwa kamati maalumu ya kupambana na israfu pamoja na kuwepo warsha maalumu kuhusiana na suala hilo.
Ayatullah Shabestar ameashiria israfu inayofanyika katika baadhi ya hafla za maombolezo na harusi na vilevile mahari ya juu na kusema mambo haya yanavuruga afya ya jamii na uchumi wa familia.
Kiongozi huyo wa kidini ametoa wito wa kufanyika juhudi za kutosha za kubainisha wazi suala la israfu na namna na kukabiliana na batili hiyo katika jamii.
395036