Gazeti la Al Wasat la Bahrain limemnukuu Katibu Mkuu wa mashindano hayo Muhammad al Hajir akisema kuwa matokeo ya mashindano hayo yatatangazwa wiki moja baada ya kumalizika.
Amesema mashindano hayo yanafanyika katika viwango vitatu vifuatavyo: Kiwango cha kwanza kitakuwa cha kuhifadhi sura za Muzzamil, Muddathir na Qiyamat. Kiwango cha pili kitakuwa cha kuhifadhi sura Shuaraa na kiwango cha tatu kitakuwa cha kuhifadhi Juzuu 22 kwa washiriki wote. Ameongeza kuwa washiriki wote wanapaswa kufahamu maana ya misamiati ya Qur'ani.
Katibu Mkuu wa Mashindano hayo Muhammad al Hajir amongeza kuwa washiriki katika mashindano hayo walianza kujiansikisha tarehe 14 Februari na kwamba kuna idadi kubwa ya waliotangaza kuwa tayari kushiriki.
Awamu ya kwanza ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu chini ya anuani ya "Abdulazizi bin Muhammad Al Khalifa" ilifanyika mwaka 1988.
Katika mashindano 21 yaliyopita washindani 3500 wakiwemo wanawake na wanaume wlishiriki katika mashindano hayo. Katika awamu ya 14 kulianzishwa mashindano ya Tafsiri, Tartil na utafiti kuhusu Qur'ani katika mashindano hayo. 395277