IQNA

Maonyesho wa Programu za Kiislamu za Kompyuta katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

12:17 - April 28, 2009
Habari ID: 1770878
Sambamba na Kongamano la kwanza la Qur'ani Tukufu na Uhusiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, kumefanyika pia maonyesho maalumu ya programu za kompyuta za Kiislamu zilizozaliswa na Taasisi ya Utafiti wa Kompyuta wa Sayansi za Kiislamu.
Sayyid Murtaza Sajadinejad anayesimamia masuala ya maonyesho katika taasisi hiyo amesema kibanda cha Taasisi ya Utafiti wa Kompyuta wa Sayansi za Kiislamu kimewavutia washiriki wengi wa kongamano hilo lililofanyika 26 Aprili.
Kongamano hilo lilifunguliwa kwa ujumbe wa Ayatullah Javad Amoli na hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bw. Monoucher Mottaki. Wasomi na watafiti wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani walihudhuria kongamano hilo.
Katika hotuba yake Waziri Mottaki amesema, kuna udharura wa mafunzo ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu kutumika katika uhusiano wa Kimataifa. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezidisha juhudi za kuarifisha mafunzo ya Qur'ani kote ulimwenguni na katika uga wa uhusiano wa kimataifa.
Mottaki amesema kongamano hilo ni juhudi za awali za kupanua utumizi wa mafundisho ya Qur'ani katika siasa za kimataifa na inatazamiwa kuwa hii itakuwa ni hatua ya kimsingi katika kuhakikisha mafunzo ya Qur'ani yanatumika kama msingi wa sheria za kimataifa. 395300
captcha