IQNA

Hatua haramu za Israel huko Qus zinakiuka sheria za kimataifa

12:36 - April 29, 2009
Habari ID: 1771299
Amr Musa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu amesema kuwa hatua haribifu za utawala haramu wa Israel katika ardhi unazozikalia kwa mabavu huko Quds Tukufu zinakiuka misingi ya sheria za kimataifa, jambo linalofanya sheria hizo kutokuwa na maana.
Kwa mujibu wa tovuti ya Quds Press, Amr Musa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na ujumbe mmoja wa Hispania huko mjini Cairo, na kuongeza kuwa Waarabu wanasisitiza kuwa hatua hizo haribifu zinazotekelezwa na Israel huko Quds hazitauongezea utawala huo haki yoyote. Amesema, unyama na ukandamizaji ambao umekuwa ukitekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia utajadiliwa na Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika kikao chao cha dharura mwezi ujao.
Katika upande wa pili, ameashiria mazungumzo ya makundi ya Palestina yanayoendelea huko mjini Cairo na kuongeza kuwa, mazungumzo hayo yanatarajiwa kupelekea kutiwa saini hati ya maelewano kuhusiana na udharura wa kuondolewa tofauti na hitilafu kati ya makundi hayo, ikiwa ni katika hatua ya kutatua matatizo na machungu ya wananchi wa Palestina. 396166
captcha