Kikao hicho kilihudhuriwa na Muhammad Amin Oiz Afshar, Mshauri wa Maziri wa Masuala ya Kidini wa Uturuki na Waislamu wa nchi hiyo wanaoishi mjini New York.
Oiz alizungumza katika kikao hicho kuhusiana na umuhimu na nafasi ya familia katika mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw) na kusema kuwa Mtume aliikomboa jamii ya mwanadamu ambayo ilikuwa inadidimia taratibu na kuiletea thamani kubwa za kibinadamu na kiutu. Amesema, Mtume alibadilisha fikra potofu za kijahili zilizokuwa zikitawala katika zama hizo na thamani za familia.
Amesisistiza kwamba iwapo mwanadamu wa leo atazingatia maisha na sira ya Mtume, bila shaka atajitengenezea maisha bora na salama na kupata kila kitu anachokitafuta humu duniani. Mashindano ya hadithi yalifanyika mwishoni mwa kikao hicho ambapo washindi walipewa zawadi. 396190