Hafla ya kutangaza kufungamana na harakati za mapamabano za Wapalestina imefanyika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirtu chini ya anwanu ya, ‘Mapambano, Chaguo la Umma, Kuondoa Mzingiro wa Ghaza Wadhifa wa Kitaifa na Kikaumu’.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, hafla hiyo imehudhuriwa na watu kutoka matabaka mbalimbali za kijamii ya Lebanon. Aidha wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Palestina walishiriki.
Walioshiriki wamesisitiza udharura wa kuendelezwa uungaji mkono wa Hizbullah kwa harakati ya wanamapambano wa Kipalestina. Wamesema mapambano ni chagua la umma wote wa Kiislamu na kwamba ni haki yao kuendeleza mkondo huo.
Fathi Yakan afisa mwandamizi wa Harakati ya Amal ya Lebanon amesema Hizbullah iliwaunga mkono wanamapambano wa Kipalestina hasa harakati ya Hamas wakati wa vita vya siku 22 vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza. Amesema suala hilo ni fahari kwa wanamapambano wote wa Lebanon.
Naye Osama Hamdan, mwakilishi wa Hamas nchini Lebanon ameshiriki katika hafla hiyo na kusema mapambano ni chaguo la umma na kila ambaye atajiondoa katika chaguo hilo basi ameondoka katika umma.
Naye Sheikh Wahab mkuu wa harakati ya Tauhid la Lebanon amesema historia haitawasamehe wale wote watakaoyasaliti mataifa yao. 396030