Kwa mujibu wa tovuti ya jumuiya hiyo, mkuu wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu amesema kuwa, mchezo huo unatusi moja kwa moja matukufu ya dini za Kiislamu na Kikristo na kwamba umetengenezwa kwa makusudi ya kuleta mfarakano miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali. Ameitaka tovuti inayoonyesha mchezo huo kuufuta mara moja na kuongeza kuwa mchezo huo hauna natija nyingine isipokuwa kuchochea hisia za wafuasi mbalimbali wa kidini na kudhoofisha moyo wa mazungumzo na usamehevu miongoni mwao.
Mchezo huo wa kompyuta unamuonyesha Mtume Muhammad, (saw) Nabii Issa (as) na viongozi wengine wa kidini wakipigana. Mtengenezaji wa mchezo huo amesema baada ya ukosoaji huo wa OIC kwamba mchezo huo umefutwa kutoka kwenye mtandao. Amedai kwamba lengo lake la kutengeneza mchezo huo lilikuwa ni kukabiliana na vitendo vya misimamo mikali na pia kupinga harakati za kuenezwa vikaragosi vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw) katika magazeti ya Denmark! 396724