IQNA

Kuanza mpango wa Uzinduzi wa Kiislamu nchini Scotland

16:05 - April 30, 2009
Habari ID: 1772034
Mpango wa Uzinduzi wa Kiislamu umeanza kutekelezwa katika mji wa Aberdeen huko Scotland.
Lengo la utekelezaji wa mpango huo limetajwa kuwa ni kuinua juu kiwango cha utambuzi na maarifa ya jamii hususan wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu dini, maisha ya Waislamu na utamaduni wa Kiislamu.
Mkuu wa Jumuiya ya Wanachuo wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Aberdeen amesema kuwa lengo la kutekelezwa mpango huo ni kuarifisha sura ya Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu na kuboresha mashirikiano kati ya wafusi wa dini hiyo na wafuasi wa dini nyinginezo.
Ajenda ya mkutano huo inajumuisha vikao vya mihadhara, maswali na majibu na mazungumzo kati ya hadhirina. Vikao hivyo ambavyo vitaendelea hadi siku ya Ijumaa ijayo vinafanyika katika Chuo Kikuu cha Aberdeen. 396096

captcha