Katibu Mkuu wa kituo hicho Adil al Saddi amesema kuwa mkutano huo utawashirikisha wawakilishi wa taasisi za kidini, kiutamaduni, kisheria na jumuiya za mahubiri ya Kiislamu na yasiyokuwa ya Kiislamu. Ameongeza kuwa wawakilishi wa jumuiya hizo watachunguza suala la kubuni hati ya kimataifa ya kuheshimu Mitume wa Mwenyezi Mungu.
Adil al Shaddi ameashiria hatua ya hivi karibuni ya vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumvunjia heshima Nabii Issa Masih (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) na akasema anatajia kwamba wawakilishi wa Vatican pia watashiriki katika kutano huo.
Kituo cha Kimataifa cha Kumuarifisha Mtume Muhammad (saw) siku chache zilizopita kilizindua mpango wa "Mabalozi wa Kumuarifisha Nabi wa Rehma" kwa kuanza kutoa mafunzo maalumu kwa walinganiaji 500 watakaokuwa na jukumu la kumuarifisha Mtume Muhammad (saw) kwa walimwengu. 398016