IQNA

Mashindano ya sauti nzuri ya kisomo cha Qur'ani kufanyika Dubai

9:49 - May 03, 2009
Habari ID: 1773027
Mashindano ya sauti nzuri zaidi ya kisomo cha Qur'ani Tukufu yanaanza leo katika mji wa Dubai kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu. Mashindano hayo yanasimiwa na kamati inayosimamia mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Zawadi ya Dubai.
Gazeti la al Khalij limeandika kuwa Mkuu wa kamati hiyo Ibrahim Bumalha amesema kuwa mashindano ya sauti nzuri zaidi ya kusoma Qur'ani yanaanza leo katika ukumbi wa Islah.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha siku tano yatahudhuriwa na wajumbe wote wa kamati inayosimamia mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Zawadi ya Dubai. Amesema kuwa mashindano ya sauti nzuri ya kusoma Qur'ani ni moja ya sehemu mpya za mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Zawadi ya Dubai. 397902

captcha