Akizungumza pambizoni mwa kikao cha Kiislamu cha nchi za Mauritania na Senegal, Rais Abdoulaye Wade amebainisha hamu yake ya kuwakusanya wanazuoni wa Kiislamu wa nchi za Kiafrika kutokana na pendekezo lililotolewa na Waislamu wa Nigeria, Sudan na nchi nyingine nyingi za Afrika. Ameelezea matumaini yake kwamba kikao cha wanazuoni wa Kiafrika kitapelekea kuandaliwa kikao kingine kama hicho cha nchi zote za Kiislamu wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC kwa lengo la kutatua matatizo na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu.
Mwenyeki huyo wa hivi sasa wa OIC amesema sababu ya kuainishwa mwaka 2010 na 2011 kwa ajili ya kufanyika vikao hivyo ni kufanyika katika vipindi hivyo vikao vya Umoja wa Nchi za Kiislamu nchini Senegal.
Kikao hicho cha maulamaa wa Kiislamu wa Senegal na Mauritania ambacho kinatazamiwa kumalizika leo Jumatatu huko Dakar, mji mkuu wa Senegal, kinafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Elimu na Kazi ya Afrika FASA.
Tarehe 13 na 14 Machi mwaka uliopita Senegal iliandaa kikao cha 11 cha wakuu wa nchi za Kiislamu. 398735