IQNA

Waislamu wa Malta Wapinga kufungwa kituo chao cha ibada

22:40 - May 03, 2009
Habari ID: 1773450
Waislamu wa mji wa Islima huko Malta wamekusanyika mjini humo na kuswali swala ya jamaa kama hatua ya kulalamika dhidi ya kufungwa kituo chao cha ibada.
Kiongozi wa Waislamu wa Malta Bader Zina amesema kuwa Waislamu hao wamekusanyika kupinga kitendo cha kufungwa kituo chao cha ibada na wametoa wito wa kufunguliwa kituo hicho mara moja. Kituo hicho kilifungwa siku kadhaa zilizopita kwa tuhuma ya kutokuwa na kibali.
Kiongozi huyo ameashiria hatua ya vyombo vya dola vya Malta ya kufunga kituo kingine cha ibada cha Waislamu na akahoji, tangu lini na wapi utekelezaji wa ibada unahitaji kibali?
Bader Zina amesema kuwa hatua hiyo ya kufungwa kituo cha ibada cha Waislamu imechukuliwa huku wafuasi wa dini nyingine wakitekeleza ibada zao na shughuli za kidini kwa uhuru kamili.
Hakuna takwimu rasmi kuhusu idadi kamili ya Waislamu katika nchi ndogo ya kusini mwa Ulaya ya Malta ingawa vyombo visivyokuwa rasmi vinasema kuwa idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu laki nne. 398778

captcha