IQNA

Maonyesho ya nakala ya Qur'ani iliyoandikwa na Imam Sajjad

7:57 - May 04, 2009
Habari ID: 1773453
Maonyesho ya nakala za kale na za kihistoria za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za waandishi na wanafikra wakubwa wa Kiislamu ikiwemo nakala iliyoandikwa kwa hati za Imam Sajjad, mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), yameanza katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq.
Ali al Khabbaz msimamizi mkuu wa maonyesho hayo amesema kuwa maonyesho hayo yanayofanyika katika haram ya Abbas bin Ali (as) yanafanyika kwa lengo la kuwaelimisha wananchi na viongozi wa Iraq kuhusu nakala za maandishi ya mkono yenye thamani kubwa ya Qur'ani.
Al Khabbaz amesisitiza kuwa kuhifadhi nakala hizo za kale na zenye thamani kubwa kunahitaji mafunzo na jumba makhsusi la makumbusho na akaongeza kuwa maonyesho hayo yataendelea kwa kipindi cha wiki moja na kwamba nakala zinazoonyeshwa ni za kuanzia karne ya kwanza hadi kuni na nne Hijria.
Ali al Khabbaz amesema kuwa vitu vingine vinavyoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na panga za kale na ala nyinginezo za kivita zilizonakshiwa kwa dhahabu na fedha na mishumaa ya shaba na viyoo ya zamani. 398561
captcha