IQNA

Mpango wa Kusoma Qur'ani wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu Washington

8:49 - May 04, 2009
Habari ID: 1773464
Mpango wa Kusoma Qur'ani Tukufu katika mtandao wa intaneti wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu mjini Washington Marekani umewavutia wengi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Intaneti wa kituo hicho, mpango huo ulizinduliwa mwaka mmoja uliopita kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Ustadh Shahid Murtadha Mutahari lengo likiwa ni kuimarisha utamaduni wa Qur'ani.
Katika mpango huo, Wasomaji wa Qur'ani wanajisajilisha kupitia mtandao wa intaneti wa kituo hicho na kisha wanajitolea kusoma juzuu moja ya Qur'ani katika muda ulioainishwa kabla.
Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kumekuwa na visomo vya Qur'ani na katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mpango huo ulikuwa ukitekelezwa kila siku. Visomo vya Qur'ani vimekuwa vikijumuisha makundi mbalimbali zikiwemo familia.
Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu mjini Washington kinatoa wito kwa wanaotaka kujisajilisha kuutembelea ukurasa wa intaneti wa www.iec-md.org ili kupata maelezo zaidi. 397671

captcha