IQNA

Jumuiya ya kuidhinisha chakula halali yabuniwa Ufilipino

8:35 - May 04, 2009
Habari ID: 1773468
Kufuatia sisitizo la Waislamu wa Ufilipino la kutumia chakula halali, serikali ya nchi hiyo imeafiki pendekezo la kubuniwa jumuiya itakayojumuisha maulamaa na wataalamu wa Kiislamu ambayo itakuwa na jukumu la kuchunguza mkondo wa uzalishaji bidhaa za vyakula halali kwa kiwango bora zaidi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika eneo la kusini-mashariki mwa Asia, Kaimu Waziri wa Biashara wa Ufilipino Thomas Aquino amesema kuwa, ‘serikali ya Ufilipiono imewateua maulama wa Kiislamu ambao watakuwa na jukumu la kuratibu mkondo wa uzalishaji bidhaa za vyakula halali’.
Ameongeza kuwa, kwa kutumia uzoefu na maulama hao Waislamu, uzalishaji bidhaa za vyakula halali utaboreshwa.
Aquino ameongeza kuwa wawekezaji wa Saudi Arabia wamewekeza katika sekta ya uzalishaji bidhaa za vyakula halali nchini Ufilipino na jambo hilo litasaidia kuinua harakati za uchumi wa Kiislamu nchini humo. 398383
captcha