IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kufanyika Thailand

17:20 - May 05, 2009
Habari ID: 1774069
Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ambayo yameandaliwa na Jumuiya ya Maqari wa Thailand yatafanyika tarehe 7-8 Mei katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangkok.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika eneo la Kusini Mashariki mwa Asia,mbali na Jumuiya ya Maqari wa Thailand, mashindano hayo pia yamedhaminiwa na Jumuiya ya Maqari Wanaowaunga Mkono Watoto Mayatima, Chuo cha Kiislamu cha Bangkok na Benki ya Kiislamu ya Thailand.
Mashindano hayo ya siku mbili yatakayowajumuisha waliohifadhi Qur'ani katika viwango vyote yatafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kiislamu cha Bangkok.
Imearifiwa kuwa, washindi katika mashindano hayo watashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Saudi Arabia yatakayofanyika katika mji mtakatifu wa Makka. 396870

captcha