Mashindano hayo ambayo yanasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia yanahudhuriwa na Amir wa eneo la Riyadh Sulaiman bin Abdulaziz Al Saud.
Amir Sulaiman bin Abdulaziz amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutoa huduma kwa nafasi aali ya Qur'ani, kuhamasisha vijana kuhifadhi na kusoma Qur'ani, kuelewa maana ya aya zake, kutekeleza mafundisho yake katika jamii na kulea kizazi chenye maadili ya Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa washindani 91 wanachuana katika mashindano hayo yanayowashirikisha wanaume na wanawake.
Amir Sulaiman bin Abdulaziz amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika katika sehemu tano zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani kamili na kisomo cha tajwid na kufasiri maana ya maneno yake, kuhifadhi Qur'ani kamili na kusoma tajwidi tu, kusoma juzuu 20 na kusoma tajwidi na kadhalika. 399259