IQNA

Mazoezi na hima, misingi miwili ya kustawi kwa maqari

9:33 - May 06, 2009
Habari ID: 1774517
Qari mmoja wa kimataifa kutoka Iran amesema anaamini kuwa mazoezi na hima ni misingi miwili muhimu ambayo maqari wanaoanza kujifunza kuisoma Qur'ani Tukufu wanapaswa kuizingatia.
Muhammad Reza Purzargari, mmoja kati ya maqari wa kimataifa wa Iran ameyasema hayo na kuongeza kuwa maqari vijana hawapasi kuridhika na kusikia visomo vya kari mmoja au wawili tu duniani.
Amesema wasomaji wanaojufunza na walio katika kiwango cha kuwaiga wengine wanapaswa kuzingatia zaidi suala la lahn ili waweze kujistawisha katika kusoma Qur'ani Tukufu. Aidha amewataka maqari kujitahidi kusoma kwa njia sahihi . 400068
captcha