IQNA

Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt (AS) ina wanachama katika nchi 114

9:48 - May 06, 2009
Habari ID: 1774518
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) amesema jumuiya hiyo ina wanachama katika nchi 114 duniani.
Hujjatul Islam Akhtari Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) ameongeza kuwa kutokana na kuwepo idadi kubwa ya Waislamu wa madehebu ya Shia ambao ni wanasiasa, wasomi, wafanya biashara na wanaoshika nyadhifa muhimu kimataifa, fursa hii inaweza kutumika kuunda mtandao mkubwa wa Mashia duniani.
Amesema Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) inajitahidi kuwaunganisha Mashia kote duniani. Sheikh Akhtari amesema kuwa hii leo katika nchi nyingi duniani kuna jamii za Mashia zinazotambuliwa rasmi na kwamba kuwaunga mkono kiutamaduni, kuwatetea na kuwahami kisheria Waislamu hao pamoja na kuongeza maarifa yao kuhusu Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (SAW) ni kati ya malengo ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS).
Mwanazuoni huyo mwandamizi wa Iran amesema, maadui wamewekeza kwa kiwango kikubwa ili kuwakandamiza Mashia. Ameongeza kuwa kutokana na baraka kubwa za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulioleta mwamko wa Kiislamu, maadui sasa wanahisi hatari na kwa hivyo wanapanga njama kubwa za kuwakandamiza Waislamu na hasa Mashia. 400134
captcha