Kongamano hilo, ambalo limeandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Zimbabwe na taasisi za Kiislamu nchini humo, litafanyika kwa mnasaba wa mwaka wa 20 wa kumbukumbu ya kuaga dunia Imam Khomeini (SA).
Kamati inayoandaa kumbukumbu hiyo imesema kutafanyika mashindano ya kiutamaduni kumhusu Imam (SA) katika magazeti ya nchi hiyo mbali na kuchapishwa makala mbalimbali katika gazeti la kila siku la Herald. Aidha kutafanyika maonyesho ya vitabu na picha za Imam Khomeini (SA). Vile vile kutaonyeshwa filamu ya maisha ya Imam (SA) katika televisheini ya Zimbabwe mbali na kusambazwa vitabu vya Kiingereza kuhusu maisha ya mwanzilishi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kamati hiyo pia imesema kutazinduliwa kitabu kiitwacho: “Imam Khomeini (SA), nyota inayong’ara ambayo kamwe haitazama’. Kitabu hicho kimeandikwa na Makari, mwandishi mkristo wa Zimbabwe na kimechapishwa na Shirika la Kimataifa la Uchapishaji la Al Huda. 400863