Muhammad Taqi Mirzajani, afisa wa mawasiliano katika Baraza Kuu la Qur'ani amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa: ‘Kwa ushirikiano wa waandalizi wa maonyesho na Baraza Kuu la Qur'ani, maqari wa kimataifa watasoma Quran katika eneo la maonyesho, Ukumbi Mkubwa wa Swala wa Imam Khomeini (SA), kwa siku kumi za maonyesho kuanzia tarehe 6 Mei’.
Ameongeza kuwa, tilawa ya Qur'ani Tukufu, adhana, na usomaji dua wakati wa adhuhuri na magharibi pamoja na kuongoza sala za Jamaa ni kati ya ratiba zilizoandaliwa na Baraza Kuu la Qur'ani katika maonyesho ya vitabu mwaka huu mjini Tehran. 400745