IQNA

Kongamano la Usahihi wa Kitabu cha Qur'ani kufanyika Uturuki

12:09 - May 07, 2009
Habari ID: 1775138
Kongamano la Usahihi wa Kitabu cha Qur'ani linatazamiwa kufanyika nchini Uturuki tarehe 9 na 10 mwezi huu wa Mei.
Kongamano hilo litakalohudhuriwa na wanafikra, maulamaa na wahadhiri wa vyuo vikuu, litajadili aya ya tisa ya suratul Hijr inayosema: "Hakika Sisi ndio tulioteremsha Qur'ani, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda".
Kongamano hilo litafunguliwa kwa kisomo cha aya za Qur'ani na kuhutubiwa na wasomi, maulamaa na wanafikra za Kiislamu.
Wasomi hao watachunguza muujiza wa Qur'ani ikiwa ni pamoja na kubakia kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu bila ya kubadilishwa wala kufanyima opotoshaji. 400781
captcha