Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand amesema umoja ni kati ya masuala muhimu katika mafundishi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, ushindi katika vita visivyo na mlingano dhidi ya makafiri ni jambo linalohitajia kuwepo umoja miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia na Sunni.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kusini-mashariki mwa Asia, Mohammad Bizmark Balozi wa Iran nchini Thailand ameongeza kuwa leo ufahamu wa idiologia ya Kiislamu umeongezeka ulimwenguni kwani walimwengu wamediriki kuwa Uislamu ndio dini pekee inayoweza kukidhi mahitaji ya dunia na akhera. Ameyasema hayo alipokutana na wanachama wa jumuiya ya wasomi waliohitimi katika Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa (SAW) cha Iran.
Mwanadiplomasia huyo wa Iran amesema vita dhidi ya makafiri havina mlingano kwani wanamiliki aghalabu ya vyombo vya habari duniani. Amesema Marekani ndio inayoongoza katika udhibiti na umiliki wa vyombo vya habari duniani.
Balozi huyo amesema kuwa jambo muhimu ni kuwa, Waisalmu wachukue hatua katika mkondo ulio sahihi ili waweze kukabiliuana na makafiri duniani. Amesema kwa kufuata mkondo ulio sawa pamoja na kuwepo umoja wa Mashia na Masunni, basi Waislamu watapata ushindi dhidi ya makafiri. 401272