Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan, hafla hiyo imehudhuriiwa na Maqari na Mahafidh elfu tano kutoka mataifa mbali mbali ambao ni vijana wakiwemo mabanati na wavulana.
Jasim al Kharafi amesema mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuwahimiza vijana na mabarobaro kuhifadhi Kitabu Kitakatifu cha Mwenyezi Mungu. Amesema mojawapo ya njia pekee ambazo vijana wanaweza kunusurika kutokana na maovu yanayoandamana na utandawazi ni kufanyika mashidano kama hayo ya Quran. Amemuomba Mwenyezi Mungu ampe taufiki ili mashindano hayo yaendelee. 401252