IQNA

Maimamu wa Jamaa kupewa mafunzo katika Chuo Kikuu cha Vienna

12:27 - May 09, 2009
Habari ID: 1775772
Chuo Kikuu cha Viena nchini Austria kimetangaza kwamba kitatoa mafunzo maalumu kwa maimamu wa swala za jamaa katika chuo hicho na kisha kuwapa vyeti rasmi baada ya kumaliza masomo yao.
Chuo hicho kimetangaza lengo la kutolewa masomo hayo kuwa ni kuwawezesha Waislamu kuchanganyika na wafuasi wa dini nyinginezo za mbinguni. Masomo hayo pia yatajumuisha masuala ya sheria na jamii. Masomo hayo ambayo yatakamilika katika kipindi cha mihula miwili yamepewa jina la 'Maimamu wa Jamaa barani Ulaya' na katika hatua ya kwanza, Chuo Kikuu cha Vienna kitawachukua maimamu 30 kutoka misikiti mbalimbali ya Austria. Washiriki wa masomo hayo wanapasa kuwa na elimu ya juu kuhusiana na masuala ya Kiislamu. Katika hali ambayo masomo ya dini ni ya lazima katika shule za Austria, lakini kuna walimu 394 tu wa Kiislamu wanaopasa kuwafundisha wanafunzi zaidi ya 50,000. Kwa msingi huo inasemekana kuwa masomo yaliyopangwa kutolewa na Chuo Kikuu cha Vienna yanaweza kusaidia sana katika kuwajumuisha Waislamu katika jamii za Ulaya. 401652
captcha