Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Wasat wasomi mashuhuri wa Qur'ani kutoka nchi za Saudi Arabia, Kuwait, Bahrain, Qatar na Pakistan walishiriki katika mashindano hayo wakiwa katika makundi mawili ya watoto na watu wazima ambao wote walikuwa ni wanaume. Mashindano hayo yaliyoanza tarehe Pili Mei yameandaliwa na jumuiya ya Qur'ani ya Dhikrul Hakim. Ayatullah Sayyid Abdallah al-Ghureifi, mwanazuoni mashuhuri wa Kishia wa Bahrain alishiriki katika sherehe hizo. Mashindano ya uandishi wa mkono wa lugha ya Qur'ani pia yaliandaliwa pambizoni mwa mashindano hayo ambapo Ali Abdul Wahid As-Shahabi ndiye aliyeibuka msindi wa mashindano hayo. 401604