IQNA

Kikao cha Wahandisi wa Nchi za Kiislamu mjini Damascus

9:45 - May 10, 2009
Habari ID: 1776052
Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Wahandisi wa Nchi za Kiislamu kinafanyika kuanzia tarehe 10 Mei huko Damascus mji mkuu wa Syria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Syria, kongamano hilo litaendelea kwa siku tatu na litajumuisha washiriki kutoka nchi kama vile Malaysia, Misri, Saudi Arabia, Libya, Uturuki, Sudan, Jordan, Palestina, Uzbekistan na Pakistan.
Kongamano hilo limedhaminiwa na Jumuiya ya Wahandisi wa Syria.
Washiriki wa mkutano huo wa kitaalamu watajadili masuala kuhusu ulindaji mazingira na uhusiano wa suala hilo na teknolojia chini ya anuani ya: 'Kulinda Mazingira na Teknolojia'. 401693


captcha